Wednesday, 8 October 2014

ni tabibu wa karibu



NI TABIBU WA KARIBU

1.   Ni tabibu wa karibu, tabibu wa ajabu
Na rehema za daima, ni dawa yake njema

Imbeni malaika sifa za Yesu Bwana
Pweke limetukuka, jina lake Yesu

2.   Hatufai kuwa hai, wala hatutumai,
Ila yeye kweli ndiye, atupumzishaye

3.   Dhambi pia na hatia, ametuchukulia,
Twenendeni na amani, hata kwake mbinguni

4.   Uliona tamu jina, la Yesu Kristu Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa, asishindwe na kufa

5.   Kila mume asimame, sifa zake zivume,
Wanawake na washike, kusifu jina lake

6.   Na vijana wote tena, wam pendao sana,
Waje kwake wawe wake, kwa utumishi wake

No comments:

Post a Comment